Kwanini wasichana hukimbia vyuo vya Ufundi?
Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha katika Mazoezi ya Vitendo KWA muda mrefu sasa, baadhi ya wadau wa elimu nchini na wanasiasa, kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikosoa elimu inayotolewa nchini kwamba imekuwa haiwawezeshi wahitimu kushindana katika soko la ajira.Pia, kutokana na uhaba wa ajira nchini, serikali na baadhi ya wadau wamekuwa wakihimiza suala la vijana kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea kuajiriwa kwenye ofisi mbalimbali. Licha ya ukweli kuwa, pamoja na sekta nyingine zote, ile ya ufundi ndiyo inayotoa zaidi fursa ya watu kujiajiri wenyewe, takwimu zinaonyesha kuwa, idadi ya wanafunzi wanaochagua kujiunga na vyuo hivyo, hasa wasichana ni ndogo mno. Mwaka 2010, kwa mfano wanafunzi waliojiunga na vyuo vya ufundi vya serikali walikuwa 897 ambapo kati yao, wasichana walikuwa 16, idadi ambayo ni sawa na asilimia 1.78. Akitangaza matokeo ya kidato cha nne ya mwaka huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa wakati huo, Profesa Jumanne Maghembe alisema ,“Id